...................
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, alifariki dunia siku ya Jumatatu, tarehe 21 Aprili 2025, akiwa na umri wa miaka 88.
Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Deodatus Balile imesema Katika kipindi cha miaka 12 ya uongozi wake kama Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika kujenga maelewano ya kidini duniani, hususan kupitia juhudi zake za kuhimiza mazungumzo ya amani miongoni mwa dini mbalimbali.
Tags
Top Stories