Header Ads Widget

Responsive Advertisement

SAMIA LEGAL AID YATOA ELIMU YA MSAADA WA KISHELIA ILI HAKI IWEZE KUPATIKANA

 

 Na Prisca Libaga, Arumeru


Mkuu wa wilaya ya Arumeru  Amir Mkalipa amewataka wananchi wa wilaya hiyo kutumia Kampeni ya Msaada wa  Kisheria ya Mama Samia katatua migogoro na malalamiko yao yanayosababishwa na kukosekana elimu ya msaada wa kisheria ili haki iweze kupatikana.

Mkalipa ameyasema  hayotarehe 31 Machi, 2025 wakati alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Damas Ndumbaro wakati wa  uzinduzi  wa Kampeni  ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia iliyozinduliwa katika kata ya Makiba wilayani Arumeru.
 
Amesema Rais Samia anastahili pongezi kubwa kwa kuja na wazo la kuanzisha kampeni hiyo ambayo inakwenda kutatua migogoro mingi ya kisheria ambayo wao kama watawala wamekuwa wakishindwa kuitatua.

" Unajua sisi kama watawala linapokuja suala la mahakama tunashindwa kuingilia kati lakini kampeni hii ina wataalam wa sheria ambao wao ndio wamekuwa wakishinda mahakamani, wamekuja kumaliza kero hizo za wananchi watawaelekeza nini cha kufanya na mwisho kila mwananchi atapata haki yake," amesema Mkalipa.

Amesema ijapokuwa siku kumi za kusikiliza kero za kisheria wilayani humo ni chache, lakini sio haba kwa kuwa sehemu kubwa ya migogoro itapatiwa ufumbuzi na wananchi watapunguza kufika ofisi za wilaya. 
Wakiwasilisha migogoro yao mbele ya Mkuu wa Wilaya wananchi wa kijiji cha Malula wamelalamikia kutaka kupokonywa mashamba ambayo wamekuwa wakiyalima tangu mwaka 1972.

Wananchi hao wamemtaja mwananchi mmoja kwa jina la Zara kuwakataza kulima mashamba hayo akidai yeye ndio mmiliki wa mashamba hayo tangu miaka ya 1960 akiyarithi kutoka kwa marehemu wazazj wake.

Mkuu wa Wilaya Amir Mkalipa aliwaeleza wananchi hao kuwa mgogoro huo anaufahamu vizuri na kwamba mashamba hayo ni mali ya Serikali na imeshayatenga kwaajili ya eneo la uwekezaji (EPZ), na kwamba hakuna mtu yoyote aliyemilikishwa.
" Mashamba ya malula ni eneo la Serikali, yameshatengwa kwaajili ya uwekezaji wa EPZ lakini kama Serikali tutakuja kuwasikiliza na tutawapanga kwa muda ili muendelee kuyalima lakini sio kuwamiliÄ·isha na watu wachache waliojenga nyumba zao zinaenda kubomolewa,"Amesema DC Mkalipa.

Kwa upande wake mkurugenzi  wa huduma za msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Ester Msambazi amesema kuwa,  Kampeni hiyo inalenga kuwawezesha wananchi kupata  huduma za mawakili  bure pamoja na elimu ya maswala ya kisheria.

Post a Comment

0 Comments