Wakati mjadala mzito wa kuahirishwa ukiendelea kuunguruma miongoni mwa mashabiki wa soka nchini ,hali ni tofauti kwa uongozi wa klabu ya Simba. Uongozi wa klabu hiyo umejikita kuimarisha ushirikiano na mashabiki wake kuelekea mchezo wa robo fainali ya kombe la shirikisho dhidi ya Al Masry yanchini misrimchezo wa raundi ya kwanza utakaopigwa April 2.
Simba wamekaa kimya katika sakata hilo na kuwaacha wapinzani wao wa jadi Yanga waendelee kupambana na Bodi ya Ligi na TFF wakati wao wakiendelea na mazoezi makali kwa ajili ya mchezo huo muhimu unaoweza kwenda kubadili historia ya klabu hiyo.
Simba yaja na mbinu za kivita kuelekea mchezo wa April 2
Uongozi wa Simba unaamini utulivu ndiyo msingi wa mafanikio ya klabu yao, Klabu hiyo ni mnufaaika mkubwa wa mashabiki wake hasa linapokuja suala la mechi za kimataifa.Si Al Ahly,Zamalek,Kaiser Chief wala Asec Mimosa anayependa kuja dimba la Benjamini mkapa kwa sababu mashabiki wa Simba wamekuwa wakileta msisimko wa kipekee kwa wachezaji wao na kuwapoteza wapinzani wao.
Kuelekea michezo ya tarehe 02 na 09 April Simba imeanza kampeni zake za kuwaweka pamoja mashabiki na hilo limefanyika kwa kuanza na kampeni ya WESE LA UBAYA UBWELA inayowataka mashabiki wa Simba kujaza mafuta katika vituo vya Lake Energies na kufanya hivyo kutainufaisha klabu kwa mapato yatakayokusanywa.
naye msemaji wa klabu hiyo Bw.Ahmed Ally amenukuliwa akisema “Hii ni bidhaa mpya ambayo Simba na Lake Energy tumeingiza sokoni. Bidhaa hii inaweza kutumiwa na Wanasimba na watu wengine. Lakini pia ni mpango maalumu wa kujitengenezea mapato. Kwa kufahamu kwamba uhitaji wa mafuta ni mkubwa nchini, Simba Sports Club tukaiona fursa kushirikiana na Lake Energy ili kuwahudumia Wanasimba lakini pia kuwawezesha kuchangia klabu yao lakini pia kwa Lake Energy kurudisha kwa Jamii.”
0 Comments