.....................
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Machi 25, 2025 amezindua lango la kuingia na kutoka watalii la Ndea kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi iliyoko Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro.
Uzinduzi wa lango hilo ambalo limegharimu Shilingi Milioni 350 ni sehemu ya maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita ili kuchochea na kuongeza vivutio vya utalii nchini.
Akitoa taarifa ya lango hilo Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi, Emmanuel Mwailama amesema ujenzi wa lango hilo utaongeza idadi ya watalii katika mbuga hiyo ambao wengi wanakwenda kuona maisha ya wanyama pembezoni mwa ziwa jipe, Faru weusi pamoja na tembo.
0 Comments