Timu ya Taifa ya Ureno chini ya Kapteni Cristiano Ronaldo imefanikiwa kutinga nusu fainali ya Ligi ya Uropa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-3 dhidi ya Denmark. Mchezo huo mgumu uliopigwa dimba la Estádio José Alvalade nchini Ureno uliibua hisia kwa mashabiki wa soka duniani kote baada ya Cristiano Ronaldo kukosa penati muhimu lakini alisahihisha makosa hayo na kufunga bao muhimu.
Tathmini ya Mchezo
Ureno waliingia vichwa chini katika mchezo huo baada ya kupoteza mchezo wa mkondo wa kwanza kwa bao 1-0 nchini Denmark kwa bao la mshambuliaji kinda Hojlund. Ureno walianza mchezo huo kwa mashambulizi makali na kujipatia penati dakika ya 6 lakini mpigaji Cristiano Ronaldo alishindwa kufunga baada ya golikipa wa Denmark Kasper Schmeichel kudaka mpira mwepesi.
Ureno walizidisha mashambulizi na dakika ya 38 Joachim Andersen wa Denmark alijifunga na kuwafanya Ureno kwenda mapumziko kwa bao 1-0. Dakika ya 56 Rasmus Kristen wa Denmar alifanikiwa kusawazisha bao.
Dakika ya 72 Ronaldo alirejesha furaha kwa mashabiki wa Ureno kwa kufunga bao la pili na kusawazisha makosa ya kukosa penati lakini Cristien Eriksen alisawazisha bao hilo dakika ya 76 na matokeo kuwa 2-2.
Kocha wa Ureno alifanya mabadiliko kwa kuwatoa washambuliaji wote wakiongozwa na Ronaldo ,Rafael Leao na na kuwapa nafasi Trincao aliyefunga mabao mawili ya dakika ya 86 na 91kisha bwana mdogo goncalo Ramos kufunga bao la 5 dakika ya 115 na kuwaondosha Denmark kwenye michuano hiyo.
Matokeo hayo yanawafanya Ureno kutinga nusu fainali ya Ligi ya ulaya wakichuana na Ujerumani katika hatua hizo,kama watashinda mchezo huo basi watatinga fainali ya michuano hiyo
0 Comments