Mlinzi wa pembeni wa Liverpool na England Trent Alexander-Arnold, 26, amekubaliana na Real Madrid kwa mkataba wa miaka mitano na atajiunga na wababe hao wa Uhispania bila malipo. (Sky Sports)
Real pia inamfuatilia winga wa Athletic Bilbao na Uhispania Nico Williams, 22, ambaye ana kipengele cha kutolewa cha euro 62m (£51.8m), iwapo nyota wa Brazil Vinicius Jr, 24, atajaribiwa na uhamisho wa kitita kinono kwenda Saudi Arabia. (Fichajes)
Manchester United inapanga kuwaruhusu wachezaji 10, akiwemo mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 27, na kiungo wa kati wa Brazil Casemiro, 33 - kuondoka kabisa katika klabu hiyo msimu huu wa joto. (Manchester Evening News)
United pia inamtazama mchezaji wa Fenerbahce Yusuf Akcicek, 19, katika kutafuta mlinzi mwingine wa kati, ingawa Tottenham Hotspur, Bayern Munich, Atletico Madrid, Napoli na RB Leipzig pia wanamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki. (Mirror)
Barcelona wanatazamia kumnunua kiungo wa kati wa Newcastle na Italia Sandro Tonali, 24, pamoja na ofa inayoweza kumnunua mchezaji mwenza wa klabu hiyo, mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 25. (Mundo Deportivo)
Mlinzi Muingereza Jarrad Branthwaite, 22, anafikiria hatma yake katika klabu ya Everton huku Manchester United na Liverpool zikimtaka. (Mirror)

Tottenham Hotspur wametoa ofa ya mapema kwa kiungo wa kati wa Sunderland Chris Rigg kabla ya dirisha la usajili la majira ya kiangazi, kwa dau la pauni milioni 37 kumnunua Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 17. (Fichajes)
Kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong anataka kusalia katika klabu hiyo na yuko kwenye mazungumzo kuhusu mkataba mpya, huku mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ukiisha 2026. (NY Times)
Mustakabali wa kiungo wa kati wa Brazil Andrey Santos, 20, katika Chelsea haujulikani, lakini anatumai kuungana tena na mchezaji mwenzake wa kimataifa Estevao Willian katika klabu hiyo ya London baada ya muda wake wa mkopo Strasbourg. Willian, 17, atajiunga na The Blues mwezi Julai kutoka Palmeiras. (Evening Standard)
Winga wa zamani wa Liverpool na Rangers Ryan Kent yuko kwenye mazungumzo ya juu ya kujiunga na Seattle Sounders inayoshiriki Ligi Kuu ya Soka. Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 28 ni mchezaji huru baada ya kuachana na Fenerbahce ya Uturuki Oktoba mwaka jana. (Sounder at heart)
0 Comments