Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali ametoa Rai kwa Wananchi Kuendelea kujiunga na kuwekeza katika hatifungani ya Zanzibar SUKUK kwa ajili ya Kupata faida halali.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Wananchi katika Futari maalumu iliyoandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar ( PBZ) iliofanyika Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Aidha Rais Dkt, Mwinyi amesema kwa kufanya hivyo Serikali itapata fedha za Kuendeleza Miradi ya Maendeleo kwa kuwa na fedha za Uhakika na Wananchi Kupata faida halali.
Rais Dkt, Mwinyi amefahamisha kuwa tayari Serikali imelizingatia wazo la kuwekeza katika Sukuk kwa Dola Hususan kwa Wazanzibar Wanaoishi nje ya Nchi (Diaspora) na sasa wanaweza kuwekeza kwa Dola.
Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameipongeza PBZ kwa Kuendelea kutoa huduma Bora za kibenki na kuifanya kuwa Benki inayoaminika na kutegemewa na Wananchi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar(PBZ) Nd, Arafat Haji amewahakikishia Wateja wa Benki Hiyo huduma Bora zinazokidhi Mahitaji Yao ya kibenki Ili kuendelea kuifanya Benki Hiyo kuwa kimbilio na Chaguo la Watu.
0 Comments