Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu Kuishi kwa kuifuata Miongozo ya Uislamu pamoja na kufungamana na Ibada.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipozungumza katika Mashindano ya Tajwiid Quraan yalioandaliwa na Taasisi ya AlHikma Quraan Foundation yà liofanyika Masjid Jamiu Zenjibar Mazizini Wilaya ya Mjini.
Aidha Rais Dkt, Mwinyi amesema Kazi kubwa inayofanywa na Masheikh na Walimu wa Madarasa ya kuwasomesha Vijana na Kuwa na Uwezo wa Kuhifadhi Quraan inapaswa kuungwa Mkono na kila Mmoja .
Amewanasihi Waislamu kushughulika na Miongozo ya Dini hiyo ili Wapate kuongoka kwani Quraan ni kitabu cha Uongofu.
Rais Dkt, Mwinyi amewahimiza Waislamu kuzidisha bidii ya kuisoma Quraan na Kuwasimamia Watoto kuwa na Mwenendo Mzuri unaonekana wakati wa Mwezi wa Ramadhani .
Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amewapongeza Wadhamini wanaoendelea kuyafadhili Mashindano hayo kila Mwaka na kuwaomba wengine wapya kujitokeza kuunga Mkono Juhudi hizo.
0 Comments