Header Ads Widget

Responsive Advertisement

RAIS MWINYI:TUDUMISHE AMANI KWA MAENDELEO ZAIDI.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewasisitiza Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuiombea Nchi Amani wakati huu ikielekea katika Uchaguzi Mkuu pamoja na Viongozi Wakuu wa Nchi .



Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipozungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu baada ya Kujumuika katika Sala ya Ijumaa, Msikiti wa Ijumaa Mpapa Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 14 Machi 2025.


Amefahamisha kuwa Maendeleo yanayofikiwa hivi sasa hapa nchini yanatokana na kuwepo kwa Amani na kuahidi kuendeleza Juhudi za kuleta Maendeleo Zaidi.


Aidha Rais Dkt.Mwinyi amewahakishia Wananchi wa Mpapa kuwa Serikali itazifanyia  Kazi Changamoto za Kijamii ziliomo katika kijiji  hicho .


Changamoto hizo zilizobainishwa na Wananchi ni Uchakavu wa Barabara za ndani , Ukosefu wa Uzio katika Skuli ya Mpapa na Ukosefu wa huduma za Karibu za Afya  kutokana na kutomalizika kwa Kituo cha Afya kiliopo kwa Miaka mingi ambacho kimejengwa kwa nguvu za Wananchi.


Vilevile Rais Dkt. Mwinyi amewahakikishia kuwa Serikali itamaliza Changamoto hizo   alizoziielezea kuwa ni za  Muhimu.

Post a Comment

0 Comments