Chelsea inaweza kuuza hadi wachezaji 11 msimu huu wa joto - ikiwa ni pamoja na Waingereza wawili, mshambuliaji Raheem Sterling, 30, na beki mwenye umri wa miaka 28 Ben Chilwell - ili kupata fedha za kununua mshambuliaji mpya. (Mail)
Arsenal wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Fiorentina Muitaliano Moise Kean, 25, ambaye hapo awali alikuwa na msimu usio na mafanikio katika klabu ya Everton. (Tuttomercatoweb)
Manchester United imeongeza washambuliaji wawili wa Bundesliga - Mslovenia wa RB Leipzig Benjamin Sesko, 21, na Mfaransa wa Eintracht Frankfurt Hugo Ekitike, 22 - kwenye orodha ya wachezaji itakaowasajili katika majira ya joto. (Sky Sports)
Man Utd pia wanavutiwa na kiungo wa RB Leipzig na Uholanzi Xavi Simons, 21, ambaye walijaribu kumsajili huko nyuma kabla ya kuhamia Ujerumani kwa mkataba wa kudumu katika dirisha la Januari. (Sky Sports)

Real Betis watakutana na Manchester United kujadili mustakabali wa winga Mbrazil Antony, 25, ambaye amefanya vyema katika kipindi cha mkopo katika ligi ya La Liga. (ABC)
Bournemouth wanamtaka beki wa kushoto wa Club Brugge raia wa Ubelgiji Maxim de Cuyper, 24, iwapo watahitaji kusajili mbadala wa beki wao wa pembeni wa Hungary Milos Kerkez, 21, ambaye anasakwa na Liverpool. (Football Insider)
Atletico Madrid wanasema mshambuliaji wa Argentina Julian Alvarez, 25, hauzwi kutokana na kuripotiwa kuwa anawindwa na Liverpool. (Kioo)
Winga wa Chelsea wa Uingereza Noni Madueke, 23, analengwa na klabu ya AC Milan ya Serie A katika majira ya msimu wa joto. (Fichajes)
Kiungo wa kati wa Lille na England Angel Gomes, 24, amegoma kwenda West Ham, licha ya klabu hiyo ya ligi kuu Enlgand kumpa mkataba wenye mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki ili ajiunge nayo pale mkataba wake na Lille utakapomam=lizika msimu huu wa joto. (Guardian)

Barcelona wanataka kumsajili tena mshambuliaji wa Argentina na Inter Miami Lionel Messi, 37, katika msimu wa joto wa mwaka 2026. (TNT Sports)
Beki wa Real Madrid Mhispania Raul Asencio, 22, anatazamiwa kusaini mkataba mpya wa muda mrefu na wababe hao wa Uhispania. (Fabrizio Romano)
Real Betis ni moja ya klabu tatu za La Liga zinazotaka kumsajili beki wa kushoto wa Leeds Junior Firpo, 28, kwa uhamisho wa bure msimu huu wa joto wakati mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Dominika utakapomalizika. (Teamtalk).
0 Comments