Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imesema hali ya upatikanaji huduma ndani ya eneo lake la kihuduma katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani ipo vizur na inaendelea kuimarika kupitia vyanzo vya uzalishaji wa maji vya Ruvu Juu na Ruvu Chini.
Akiongea na Waandishi wa Habari, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire Amesema kuwa vyanzo vya uzalishaji maji katika mitambo ya Ruvu Juu na Ruvu Chini inapokea maji ya kutosha na hali ya maji katika Mtoni Ruvu iko katika hali nzuri ya uzalishaji ukiacha changamoto ndogo iliyojitokeza katika Mtambo wa Uzalishaji Maji wa Ruvu Juu ambayo imeshatatuliwa na uzalishaji unaendelea vizuri.
Mhandisi Bwire ameongeza kuwa kazi inayoendelea kwa sasa ni kuhakikisha Maji yanayozalishwa yanasukumwa nakusambaza kwa Wananchi.
Amebainisha kuwa kwa maeneo yaliyokuwa na changamoto ya huduma ikiwemo Kinyerezi, Makabe, Mshikamano na Machimbo kazi ya usambazaji maji kwa sasa inaendelea vizuri na huduma inaendelea kuimarika.
0 Comments