Ryan Giggs anadaiwa mshahara wa pauni 40,000 kwa wafanyakazi baada ya mgahawa wake kuharibiwa ghafla.Takwimu mpya zinaonyesha kuwa wafanyakazi 22 wanamdai nyota huyo baada ya kuacha kazi Biashara hiyo inadaiwa jumla ya £495,145 kulingana na Taarifa rasmi kuhusu kuanguka kwa kampuni iliyowasilishwa kwa Companies House siku chache zilizopita.
Mgahawa wa George's Dining Room na Baa yake iliyo karibu na , karibu na Manchester, vilifungwa 'papo hapo' mnamo Februari na biashara nyingine zilifutwa kwa hiari.HMRC inadaiwa takriban £117,000 kwa michango ya kodi na Bima ya Kitaifa, kuna bili ya gesi ya £15,000 na £35,000 kwa benki ya Nat West.
Ryan Giggs alifungua mgahawa na marafiki zake Kelvin Gregory na Bernie Taylor mnamo 2014 .Taylor anadaiwa karibu £13,000 na Gregory zaidi ya £53,000.Giggs hapo awali alizungumza kuhusu jinsi ukumbi huo ulivyotimiza moja ya ndoto zake za maisha ya kufungua mgahawa na marafiki zake wa shuleni . Watatu hao walikuwa wamesema walitaka kusaidia kufanya Worsley kuwa 'sehemu sahihi kwa chakula'.
Ryan alisema wakati huo, 'Tumefahamiana kwa miaka 30, na kila mara tulisema itakuwa nzuri kufanya kitu kama hiki pamoja.'Sisi sote ni vijana wa ndani na tumeishi katika eneo hili maisha yetu yote kwa hivyo tulitaka kufanya kitu huko Worsley na tunafikiri tuna toleo tofauti kabisa kwa eneo hilo.'
Tangu alipozindua George's, Ryan pia ameungana na mchezaji mwenzake wa zamani Gary Neville na kuunda kundi la GG likiwa na maana Gigs and Garry lenye umiliki wa Hoteli huko Old Trafford, na kisha Hoteli ya nyingine iko katika Soko la Hisa katikati mwa jiji.
0 Comments