Header Ads Widget

Responsive Advertisement

NILIMUITA YESU MARA TATU AKANIOKOA

 

Kunti Abdallah ambaye ni miongoni wa manusura wa poromoko la jengo la Kariakoo ambalo limesababisha vifo vya watu 31 na wengine 88 kujeruhiwa kwenye tukio hilo ambalo limetokea Jumamosi ya Novemba 16 ametoa ushuhuda juzi kwenye mkesha wa maombi uliofanyika katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Tanzania (KKKT) ushirika wa Kinondoni Dar Es Salaam.

"Niliita Yesu mara tatu, nikaanza kusikia maporomoko ya kifusi yakianguka juu ya mwili wangu. Nikasikia uzito na kila kitu kikanielemea."

Alisema aliendelea kuomba akiwa ndani ya kifusi ilhali amebanwa mwili mzima na baada ya muda alipata ujasiri wa kufungua macho na kuona nafasi ndogo iliyojitengeneza na kusaidia kumwingizia hewa.

"Nilianza kupata hewa nikaanza kumshukuru Mungu na kuimba nikiomba Yesu asinipite, Namshukuru Mungu walikuja vijana wabeba mizigo ambao waliniambia walikuta mguu wangu unacheza na walisikia sauti kwa mbali nikiimba.

"Kama si kumwita Yesu nisingepona, mimi nilikuwa mwisho kabisa wa jengo" alisema Kunti aliyeokoka miaka mitatu iliyopita.

Post a Comment

0 Comments