Header Ads Widget

Responsive Advertisement

MIAKA 30 JELA MWALIMU KUZINI NA MWANAFUNZI

 

Mahakama ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Mwalimu wa Shule ya Sekondari Nguno iliyopo wilayani humo, Subiri Andson (37) baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mwanafunzi (17).

Kesi hiyo namba 28803/2024 ilikuwa inasikilizwa na Hakimu Mfawidhi Mkazi wa Mahakama hiyo, Robert Kaanwa, ambapo mwalimu huyo alifishwa mahakamani hapo Oktoba 16, 2024 baada ya kukamatwa akiwa na mwanafunzi huyo nyumbani kwake.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Kaanwa alisema kuwa upande wa mashtaka uliwasilisha mashahidi sita na kielelezo kimoja, ambapo ushahidi huo umemtia hatiani mwalimu huyo bila ya kuacha shaka.

Awali akisoma kosa lake mahakamani hapo, mwendesha mashtaka kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilayani hapo, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Jaston Mhule alisema mshtakiwa alitenda kosa hilo Oktoba 7, 2024.

Alisema kuwa katika kijiji hicho cha Nguno wilayani humo, maeneo ya Shule ya Sekondari ya Nguno, mshitakiwa alimbaka mwanafunzi wa sekondari nyumbani kwake, chumbani.

Aliendelea kwa kueleza kuwa tarehe hiyo mshtakiwa aliwekwa chini ya ulinzi wa wananchi baada ya kumkamata akiwa na mwanafunzi huyo chumbani kwake majira ya saa moja usiku na baada ya kumkamata walimfikisha kituo cha Polisi Itilima.

Post a Comment

0 Comments