Header Ads Widget

Responsive Advertisement

MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI

 

Katika kuadhimisha siku ya UKIMWI duniani, Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Victoria Mwanziva kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amewasihii wananchi wa Mkoa wa Lindi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa UKIMWI kwani hali ya maambukizi kwa Mkoa wa Lindi imependa kutoka  0.3% hadi 2.6% .

"Kutokana na tafiti zilizofanyika imeonekana maambukizi ya UKIMWI yamepanda kutoka asilimia 0.3 kwa mwaka 2016-2017 hadi asilimia 2.6 kwa mwaka 2022-2023. Hali hii imesababishwa na shughuli nyingi za kiuchumi zilizoongezeka na muingiliano mkubwa wa watu unaosababishwa na ongezeko la maeneo hatarishi ya maambukizi ya VVU mfano maeneo ya machimbo ya madini" 

Wito huo ameutoa leo Desemba 1, 2024 katika kijiji cha Nahukahuka Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi, Mhe. Victoria amesema kuwa maambukizi hali ya maambukizi inaongezeka kutokana na shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo madini .

Aidha,  amezitaka halmashauri zotena wadau wa afya  kuongeza vitendanishi na dawa za ARV katika vituo vya kutolea hudima za afya  ili wananchi wapate fursa ya kupima afya zao na  kuweza kufahamu hali zao kwa lengo la kuchukua hatua zinazofaa kulingana na hali zao na kupata dawa bila usumbufu

"Napenda kutoa rai kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Lindi, Wadau wa maendeleo pamoja na Bohari ya kanda Kusini ya dawa mhakikishe vitendanishi na dawa za ARV zipo za kutosha katika kila kituo cha kutolea huduma katika Mkoa wetu.

 Pia, nahamasisha watu wote watakaogundulika na maambukizi ya VVU kuanza dawa mara moja ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza kiafya kwa kukosa au kuchelewa kuanza dawa mapema.

Post a Comment

0 Comments