Hali ya maabukizi ya virusi ya ugonjwa WA UKIMWI Mkoa wa Lindi imeongezeka kutoka 0.3% mwaka 2016-2017 na kufikia asilimia 2.6% mwaka 2022-2023 Hali iliyosababishwa na shughuli za kiuchumi
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bi.victoria Mwanziva akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Lindi akizungumza wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika huko Katika kijiji cha Nahukahuka halmashauri ya Mtama amewasihi wananchi Mkoani Humo kuendelea kuchukua tafadhari juu ya ugonjwa huo
Mwanziva Amesema Hali hiyo imesababishwa na shughuli nyingi za kiuchumi zilizoongezeka na muingiliano mkubwa wa watu unaosababishwa na ongezeko la maeneo hatarishi ya maambukizi ya VVU mfano maeneo ya machimbo ya madini
Aidha, amezitaka halmashauri zotena wadau wa afya kuongeza vitendanishi na dawa za ARV katika vituo vya kutolea hudima za afya ili wananchi wapate fursa ya kupima afya zao na kuweza kufahamu hali zao kwa lengo la kuchukua hatua zinazofaa kulingana na hali zao na kupata dawa bila usumbufu
"Napenda kutoa rai kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Lindi, Wadau wa maendeleo pamoja na Bohari ya kanda Kusini ya dawa mhakikishe vitendanishi na dawa za ARV zipo za kutosha katika kila kituo cha kutolea huduma katika Mkoa wetu.
Pia, nahamasisha watu wote watakaogundulika na maambukizi ya VVU kuanza dawa mara moja ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza kiafya kwa kukosa au kuchelewa kuanza dawa mapema.
0 Comments