Header Ads Widget

Responsive Advertisement

WASICHANA WATAKAO PANGIWA MBWARA SEKONDARI WATAKAA HOSTELI

Katika mkakati wa kufuta mimba mashuleni, wazazi na walezi Wa Mbwara sekondari wamekubaliana kuwa wasichana wote wanaopangiwa kusoma katika Shule hiyo kulazimika kukaa hosteli badala ya kupanga mitaani.


Maku itbaliano hayo yamepitishwa kwenye kikao Cha wazazi/walezi walimu, na Balozi wa Elimu wilaya ya Rufiji ambaye pia ni katibu wa mbunge Ndug Bashiri Kibopo akiambatana na wanachama wa TAYEF siku ya Jumatatu ya tarehe 12/8/2023 katika viwanja vya Shule hiyo ya Mbwara sekondari.


Moja ya wazazi hao alisikika akisema  " ipitishwe Sheria ya watoto wote wasichana wanaofaulu kusoma Mbwara wawe bwenini, kipengele hiki yaweza kutuma manusura kama tungeweza kutengeneza kumi na nne kwa mwaka tunaweza kubakiwa na Moja au wawili kwa sababu bwenini hapa Kuna usalama" 


Kwa upande wake Balozi wa Elimu Bashiri Kibopo amewataka wazazi kuacha tabia ya kumaliza kesi za mimba majumbani na badala yake watoe ushirikiano kwa vyombo husika ili kuweza kutokomeza mimba mashuleni kama walivyokibaliana.


Vile vile  TAYEF imetoa walimu wawili katika Shule ya sekondari Mbwara, ili kuongeza nguvu kwa Madarasa ya mitihani katika kipindi hiki Cha mwisho kuelekea mitihani wa taifa.


Shule ya sekondari Mbwara kwa sasa inauhitaji wa Bweni la wavulana ili kuepusha wimbi la kukaa kwa wanafunzi nje ya Shule bila uangalizi na hatimaye kusababisha uvutaji wa bangi na mimba mashuleni.


Katika hatua nyingine  team hiyo ya TAYEF ilifika katika Shule ya msingi Ikwiriri ambapo pia waliweza kuzungumza na wazazi pamoja ja walimu lengo kukuza kiwango Cha ufaulu katika Shule hiyo.


Wazazi pia wametoa shukrani kwa kupatiwa walimu watatu katika kuongeza nguvu kwa darasa la saba na lanne,  na kuomba ifikapo January 2025, walimu hao wafikishwe shuleni hapo Mapema ili waweze kufaidika zaidi, huku wakisisiza kuwa matokeo ya darasa la saba hayaridhishi.


Shule ya msingi Ikwiriri Ina kumla ya wanafunzi elfu mbili miamoja arobaini na sita, wasichana ni 1042 na wavulana 1104 ikiwa na jumla ya walimu 20. Na Shule ya sekondari Mbwara inazaidi wanafunzi 500

Post a Comment

0 Comments