Header Ads Widget

Responsive Advertisement

USIKUBALI KURUDI NYUMA WEWE, TAFUTA MBINU MBADALA.

Bwana Yesu Asifiwe.
Ni watu wanne ambao waliokuwa wamembeba mgonjwa wa kupooza walimwendea Yesu wakitarajia uponyaji wa mgonjwa wao lakini bahati mbaya walipofika walikutana na umati wa watu ukiwa umemzunguka na haikuwezekana kumfikia kabisa.
Badala ya kurudi nyumbani na kukata tamaa watu hawa walitafuta mpango wa pili ili kufanikisha, walipoona ameingia ndani ya nyumba walimbeba na kumpitisha Darini na baadaye akapata kuponywa.

Marko 2:3-5
[3]Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne.
[4]Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza.
[5]Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.

HATA WEWE LEO HII HUNA SABABU YA KUKATA TAMAA KWA SABABU YA MPANGO WA KWANZA KUTOKWENDA SAWA, UNAHITAJI KUTOBOA DARI YAKO UPATE KUIPATA HAJA YAKO.
Usione gharama kubwa kupangua matofali kwa ajili ya kuifuata haja yako kwani wale wanne wangerejea nyumbani wangebaki na mgonjwa wao hata wewe usikubali kurudi nyuma bila ushindi.
Umefeli kwenye maombi wewe mwenyewe fanya mpango kazi wa pili nenda kaombe na wapendwa usikubali kuacha maombi, umefeli kwenye maombi binafsi nenda kafunge na kuomba usikubali kutopata matokeo.

Kama Eliya aliomba mara saba ndipo wingu la mvua likaonekana hata wewe usiache kujaribu haijalishi haujaona matokeo bado, usikubali kukaa kimya bila mpango wa kando.
Kila unalolifanya linapofeli usikate tamaa na kurudi nyuma ila simama utafute namna tofauti ya kulifanya, ukiona halifanikiwi nenda kafanye jambo jingine hadi upate matokeo.
Umati uliowazuia wale wanne wasione matokeo , unaweza kuwa ni hofu ya kufanya, maneno mabaya na ya kukatisha tamaa, vita unavyokutana navyo, upinzani binafsi, historia za nyuma, na mambo mengine mengi lakini simama ubadili mpango na utafanikiwa.
UNAPOFELI SIO WAKATI WA KURUDI NYUMA ILA NDIO WAKATI WA KUTAFUTA MPANGO MPYA WA KUFAULU.
@MsemajiwaInjili nikutakie siku njema.

Post a Comment

0 Comments