Na Halima Kisoma, Rufiji.
Balozi wa pamba nchini Ndug Aggrey Mwanri amewataka wakulima waliobadilisha matumizi ya sumu ya kuua magugu kwa ajili ya maandalizi ya kilimo cha pamba na kufanyia kilimo kingine kuzirejesha haraka, watakaoshindwa kuzirejesha hatua za kisheria zitachukuliwa.
Hayo ameyasema Leo Ijumaa tarehe 2 August 2024 katika mkutano na wakulima wa zao hilo uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya serikali ya Kijiji Umwe kati, Ikwiriri Rufiji mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya kufuatilia Maendeleo ya kilimo hicho Cha pamba.
Barozi amewataka wakulima wa kilimo Cha pamba kuzingatia maelekezo waliopewa awali katika uandaaji wa mashamba, upandaji Hadi kuvuna zao hilo la pamba ili kuweza kuvuna mazao mengi na yaliyo bora.
Aidha barozi Mwanry ametoa Rai kwa wananchi wa Wilaya ya Rufiji kuendelea kujitokeza katika kilimo Cha zao hilo walau Kila mwananchi awe amelima heka moja ya zao hilo la pamba.
Sambamba na hilo Balozi Mwanri amesisitiza kuwa Maandalizi ya shamba yanatakiwa yaanze mapema, ili kuweza kuzalisha pamba zenye viwango huku akiwataka wananchi kuacha tabia ya kichanganya mazao katika shamba la pamba.
Kwa upande wake mwakilishi wa kampumi ya pamba Rufiji (Rufiji Cotton) Ndug Mkono amewatoa hofu wakulima wa zao hilo kuwa pamba zote zinazozalishwa watalipa kwa wakati na hakuna mkulima atakaye chelewa kupata malipo yake au kubaki na pamba yake.
Pia Ndugu Mkono amesema kuwa kwa mashamba ya wakulima yaliyokumbwa na mafuriko baada ya kupulizia sumu ya kuua magugu, hawatadaiwa malipo yoyote ila tu kwa wale ambao hawajapitiwa na mafuriko ndio watakao katwa baada ya mavuno.
Nae Afisa Pamba Bi. MECKRIDA BUNDALA katika taarifa yake ya Maendeleo kwenye kata yake, amesema kuwa chanagamoto kubwa inayosumbua wakulima kwa sasa ni mifugo kuingia kwenye mashamba ya wakulima, huku akiimbo serikali kupitia Barozi wake kuweka kipaumbele jambo hilo ili kuweza kutatua chanagamoto hiyo.
Tani 2.5 za mbegu zimetolewa katika kata ya Umwe , ambapo Awali Eka zilizo kadiriwa kulimwa, katika kata ya Umwe ni 294, Ekari zilizopata mafuliko 80, Eka zilizolimwa 15, Ekari zilizosalimika mpaka Sasa 15, na katika awamu ya pili (mlao) Ekari ambazo zilitarajiwa kulimwa 94, Eka zilizo limwa mpaka sasa.
0 Comments