Header Ads Widget

Responsive Advertisement

RAIS DKT. MWINYI AWATAKA VIJANA KUJIAMINI NA KUJITOKEZA KUWANIA NAFASI ZA UONGOZI

 

KUELEKEA Uchaguzi Mkuu mwaka 2025, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka vijana nchini kujiamini na kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi na kuwaepuka watu wanaowakatisha tamaa.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo wakati akifungua hafla maalum ya vijana iliyoandaliwa na. Global Youth Empowerment na kufanyika katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mjini Magharibi Unguja.

Amesema kuna haja ya vijana kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za Udiwani, Uwakilishi na ubunge na hata nafasi za uongozi katika vyama vya siasa.

"Tumeshuhudia kuwa Vijana wanaweza wakipatiwa nafasi hivyo ni vyema mkajitokeza kwa wingi kuwania nafasi za Uongozi," amesema Rais Dkt. Mwinyi.

Aidha Rais amesema serikali itaendelea kuhakikisha vijana wanapata elimu iliyo bora ili kukuza ujuzi na ustadi.

"Tutahakikisha vijana wanapata elimu bora ambapo tumeanza na kuboresha mifumo na miondombinu ya Elimu unguja na Pemba," amesema.

Aidha amesema kuwa, Serikali itaendelea kuweka mazingira yaliyo mazuri kwa Wawekezaji ili kuchochea ongezeko ajira kwa vijana.

Mapema Mwanzilishi wa Global Youth Institute Amina Sanga aneeleza kuwa hafla hiyo ambayo hufanyika kila mwaka ina lengo la kuhamasisha vijana kufikia maleno yao.

Post a Comment

0 Comments