Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Morocco na Misri zatinga nusu fainali Kwenye Mashindano ya soka ya Olimpiki 2024

 

Afrika itakuwa walau na medali moja katika mashindano ya soka ya Olimpiki ya wanaume baada ya Misri na Morocco zote kutinga nne bora.

Morocco ilianza na mafanikio maradufu kwa ushindi murua wa 4-0 dhidi ya Marekani kwenye uwanja wa Parc des Princes mjini Paris.

Mkwaju wa penalti kipindi cha kwanza wa Soufiane Rahimi - bao lake la tano kwenye michuano hiyo - uliipa Atlas Lions fursa ya kuongoza hadi wakati wa mapumziko.

Lakini katika kipindi cha pili ambacho kilionekana kuwa na bahati ya mtende kwao, Ilias Akhomach, nahodha Achraf Hakimi na penalti nyingine iliyofungwa na Mehdi Maouhoub ilimalizia mambo kwa mtindo wa kipekee.

Katika marudio ya mechi ya hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia la Qatar 2022, Morocco sasa itamenyana na Uhispania mjini Marseille Jumatatu (16:00 GMT) kuwania nafasi ya kutinga fainali.

Baada ya mechi hiyo, Hakimi alisifu uungwaji mkono mkubwa wa Morocco ambao umeisaidia timu hiyo nchini Ufaransa.

"Mashabiki wamekuwa wakitufuatilia katika mashindano yote," alisema mlinzi huyo ambaye anachezea soka uwanja wa Parc des Princes klabu la Paris St Germain.

"Natumai wanaweza kutufuata hadi fainali. Tunataka kuwafanya wawe na fahari."

Post a Comment

0 Comments