Waumini wengi walio wakristo au hata ambao siyo Wakristo, wanapopita katika majaribu au masumbuko katika maisha yao huwa wanapoteza Neno la matumaini wamesahau kuwa kila jambo nawakati wake.
WARUMI 15:13
Mungu wa Tumaini { imani } atujaze sisi, Kama hauna tumaini Mungu hawezi kufanya kitu kwako, ili Mungu aweze kufanya kitu kwako anaangalia Tumaini { Imani} ndani yako, Unapokuwa na Tumaini unaweza kufanikisha chochote kile kigumu kwenye maisha yako
*MATUMAINI;- Ni nguvu inayo inayo tupeleka katika ahadi za Mungu
*Matarajio katika jambo fulani
*Usiruhusu mtu aondoe Tumaini lako kwenye maisha
Daniel 3:1
Kwenye maisha ukitaa kufanikiwa labda pengine unataka kuoa,kujenga nyumba,au kufanya biashara, Lakini umejaribu kuwa shirikisha marafiki zako na haujui pakuanzia angali baada ya kushirikisha rafiki zako waka kupa majibu ya ambayo huya elewi na ukaanza kufadhaika kitu ambacho umekosa hapo ni NENO LA MATUMAINI
Kwenye maisha unatakiwa kuangalia ni watu wa aina gani na wenye huruka gani, wanakushauri nini, je watu uliokuwa nao kwenye mzunguko wa maisha yako Unaendana nao kihali ya maisha basi hao hawakufai kwa sababu hawata kushauri vyema, Usiambatane nao.
Unaweza ukawa unamalengo ya maendeleo pia unamawazo makubwa ya kimaendeleo lakini ukashindwa kufanikiwa katika mawazo na malengo yako, Hii ni kwa sababu watu walio kuzunguka mnalingana kila kitu basi jua hata ushauri wao hautakuwa mzuri na kukupelekea kukosa NENO LA MATUMAINI, Ushauri wangu nakusihi ambatana na watu waliokuzidi uwezo kibiashara,walio oa, wanaofanya vizuri kwenye kila kitu na usi kubali mtu aondoe tumaini lako kwenye maisha yako, Angali Mungu anasema nini kwenye maisha yako.
HESABU 13:17-33
Mbali na kushirikisha watu kuhusu unachotaka kukifanya na ukawaomba ushauri nakusihi MTUMAINI MUNGU
MUNGU ANAFANYA KWA WAKATI SAHIHI
LUKA 7:11-19
Watu wengi wanapitia mateso kwenye maisha yao baada ya kupoteza biashara, kazi baada ya kupoteza kila kitu anakuwa kwenye hali ya kumsahau Mungu na kukosa NENO LA MATUMAINI, Tunasahau kwamba Mungu anafanya Kwa wakati sahihi, Unachotakiwa kufanya ni kuwa na Neno la Matumaini ndani yako, Unataka kufanya biashara, Umeomba kazi, Unataka kuoa au unataka kufanya chochote kile
SWALI:- Je, Ndani ya Moyo wako unaona nini?
Unacho kiona ndicho kitakacho kuwa kwa sababu Mungu anakuwa ameona Tumaini ndani yako, Chochote kinachotokea kwenye maisha yako ni kwa sababu Mungu anataka kujitukuza kwako Mtumaini Mungu { Weka Imani kwaké
Kuna baadhi ya Mambo yanatokea au kuyafanya kwenye maisha yetu tuna msingizia shetani, mpaka shetani nayeye anashangaa { Mshitaki Wetu } ,anakwenda mbele za Mungu kukushitaki kuhusu kusingiziwa, Neno moja nakupa "Watu wangu wanaangamia kwa kuso maarifa"
Tunashindwa kumuona Mungu wakati anataka kutubariki kwa sababu Mungu haoni kitu ndani yetu, Mungu haoni TUMAINI LETU,
MASWALI YA KUJIULIZA
*Tunawaza nini kwa Bwana?
*Tunawaza nini kwenye maisha yetu?
*Tunawaza nini katika kazi Mungu
Acha kujiwazia mambo mabaya kwenye maisha yako kwa sababu mambo mabaya yanaondoa NENO LA MATUMAINI
Mungu wetu yuko SMART, Mungu wetu ni Mungu Mwenye utaratibu, Tufanye mambo kwa utaratibu unaofaa
Barikiwa sana, AMEN,
Mchungaji: Eligiver Prosper
C.A.G BETHEL CHRISTIAN CENTER
MOBILE: 0620501178.
0 Comments