Mwimbaji maarufu wa Nyimbo za Injili nchini Dkt Tumaini Msowoya amewaomba waumini wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT,)Muwimbi, Usharika wa Ifunda kuendelea kuliombea Taifa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu, mwakani.
Dr Msowoya ametoa Rai hiyo Leo aliposhiriki ibada ya Harambee ya ujenzi wa kanisa la Kisasa Leo katika kanisaa la KKKT Muwimbi .
Alisema kuwa Taifa linaelekea kwenye Uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu na Uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani hivyo jukumu kubwa la Kila mtanzania kwa Imani yake kuendelea kuombea zoezi hilo.
Pamoja na kuliombea Taifa, amewakumbusha kujiandikisha kwenye daftari la Kudumu la mpiga kura na kuendelea kuiunga mkono Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan.
Msowoya ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa amesema kuwa Chama tawala kimefanya mambo mengi mazuri chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa awamu ya sita Dr Samia Suluhu Hassan hivyo zawadi Pekee kwa serikali na Chama ni kuendelea Kuiunga mkono kwa Kuchangua viongozi wanaotokana na CCM .
0 Comments