Kuwaunganisha DJS wote wenye taaluma mbalimbali nchini kuwa kitu kimoja,
Kujenga uhusiano wa Djs ambao ni wanachama wa Tanzania Professional Djs Associational (TPDA) na BASATA kwa kufanya kazi kwa maslahi mapana ya DJS kwa ushirikiano na BASATA pamoja na Wizara.
Kuhakikisha kwamba Shughuli za Djs zinaendeshwa ili kuendana na matarajio ya DJS kupata kipato kutokana na Kazi yake na pia kuendana na serikali yenye maono kwamba Djs anatoa mchango kwenye ukuaji wa uchumi na uzalishaji wa ajira nchini;
Kuhakikisha DJS wa Tanzania anaendana na mahitaji ya wakati uliopo na ujao unaoongozwa na TEHAMA na unakuwa ni sehemu ya mabadiliko hayo kwa kuhakikisha kazi za Djs wa Tanzania zinanufaika na mabadiliko hayo, kutokana na namna ya kujitangaza na kupata mapato pia Kutengeneza mbinu za kuwepo na mashirikiano (Smart Partnerships) katika kukuza sekta ya Muziki na ukizingatia utandawazi hivyo Chama kwa kushirikana na Wasanii na wadau mbali mbali wa muziki Tanzania na nje ya nchi , tutahimiza, tutahamasisha na kuratibu mashirikiano hayo baina MA DJS na Vyama vingine na Mashirikisho ambavyo ni ya ndani au nje ya nchi kwa lengo la kukuza na kuleta ustawi kwa wanachama wetu.
Kujenga uhusiano wa kindugu kwa DJS ambao ni wanachama wa TPDA na pia kujenga na kuimarisha Uhusiano kati ya Madjs mbalimbali nchini na nje ya nchi .
Kuandaa mafunzo mbali mbali kuhusu shughuli ya DJS na maendeleo yao kwa kushirikiana na wadau wa Muziki ikiwemo BASATA, COSOTA, Wizara na wataalam wengine mbali mbali wanaoendesha mafunzo ilikuwapa wanachama wetu na wengineo elimu kuhusu udj, masuala ya sheria za sanaa, masuala ya haki miliki/shiriki, masuala ya kodi, elimu kuhusu ujasiriamali Afya, Mazingira utalii na kadhalika kwa manufaa ya mwanachama na kazi zake;
Kuandaa Tuzo za DJS kwa lengo la kuenzi mchango wa Madjs na kuwapa hamasa Djs wanachama na kizazi kipya na itasaidia kuendeleza Tasnia ya DJS Tanzania
0 Comments