Header Ads Widget

Responsive Advertisement

TAMASHA LA KIZIMKAZI KUANZA AGOST 18 HADI 25 MWAKA HUU

 

TAMASHA la Tisa la Asili ya Watu wa Kizimkazi linatarajiwa kufanyika Agosti 18 hadi 25 mwaka huu ambalo linatajwa kuwa moja ya  kichocheo cha ukuaji wa Uchumi wa Nchi.

Tamasha hilo awali lilifahamika kama Samia Day na lilianza rasmi 2016.

Akitoa taarifa kwa vyombo mbalimbali vya Habari, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo Mahfoudh Said Omar amesema kuwa, Tamasha hilo kwa mwaka huu litadumu kwa siku saba na kushirikisha shughuli za Kimila,kijadi, utamaduni na uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

"Niwahakikishie Wananchi kuwa Mwaka huu mtoto hatumwi dukani maana kutakuwa shughuli mbalimbali, " amesema.

"Kutakuwa na siku ya taarabu asilia, usiku wa ngoma assilia,usiku wa bongo fleva na usiku wa vichekesho," ameeleza.

Hata hivyo ameeleza kuwa kutakuwa na mashindano ya mashindano mbalimbali ya kuibua na vipaji kwa vijana.

Mapema Katibu wa Tamasha hilo Hamid Abdulhamid Khamis amesema kuwa, katika Tamasha hilo litahusisha pamoja namafunzo ya kwa Vijana zaidi ya 500 na uzinduzi wa kituo cha Michezo Samia Suluhu Hassani.

Kwa upande wao Wafanyabiashara katika eneo la Kizimkazi wameeleza kuwa uwepo wa Tamasha hilo linawanufaisha kwa kuuza biashara zao kwa wingi na kukuza vipatp vyao.

Tamasha la Kizimkazi limekuwa kivutio kikubwa kwa Wananchi wa Kusini pamoja na wageni kutoka Zanzibar na Nje ya Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments