Makala ya Uri Silberscheid, profesa wa falsafa ya siasa na sheria katika Chuo Kikuu cha Haifa, anaona dalili zote zinaonyesha Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu hana nia ya kumaliza vita huko Gaza.
Silberscheid anasema, Netanyahu hakatai hilo, akielezea kile ambacho waangalizi wengi wakiwemo majenerali wastaafu wa Israel, wanakieleza; nacho ni kukataa kwake kuandaa mpango wa kupata mbadala wa Hamas huko Gaza.
Silberscheid anasema Netanyahu anataka kuiweka Israel kwenye mtego wa serikali ya mrengo wa kulia kwa muda mrefu zaidi, ili kuhakikisha yeye mwenyewe anaendelea kuwa madarakani.
Ili Netanyahu afanikishe hilo, ni lazima kuwa na maadui wa nje. Atafanya kila kitu ili vuguvugu la Wapalestina, Hamas libaki kama lilivyo, ili libakie kama adui wake wa milele.
Netanyahu pia amefanya kazi ya kudhoofisha Mamlaka ya Palestina kwa nia ya kuimarisha Hamas, hata katika Ukingo wa Magharibi, kwa lengo la kudhoofisha nguvu yoyote kubwa ambayo inaweza kuwa mbadala wa Hamas katika Ukanda wa Gaza.
Silberscheid anasema Israel chini ya uongozi wa Netanyahu, haitafuti kuchukua fursa ya ushindi wake katika eneo la Gaza ili kuiweka serikali mbadala wa Hamas, na kurekebisha uhusiano na Saudi Arabia, au kuunda uhusiano na mataifa ya ki-Sunni yenye msimamo wa wastani dhidi ya Iran.
Silberscheid anasisitiza: Hivi ndivyo hasa Netanyahu anavyotaka, na vita vya upande wa kaskazini vitaleta lengo hilohilo.
Kwa kuwa kufikia makubaliano ya kuwaachilia huru watu waliotekwa nyara kungekomesha vita, jambo ambalo Israeli inalihitaji, Netanyahu anasimama kuwa kizuizi cha kufikia mapatano hayo.
0 Comments