Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Kwa nini afya ya utumbo ni muhimu na unawezaje kuiboresha?

 


Utafiti unaonyesha afya ya utumbo inaweza kuhusishwa na kila kitu kutoka viwango vya mafutamafuta mwilini hadi msongo wa mawazo.

Na kadri ufahamu wetu kuhusu jukumu la kiungo hiki muhimu unavyoongezeka, ndivyo pia hamu ya afya nzuri ya utumbo unavyoimarika.

Soko la kimataifa la probiotics lilifikia karibu dola za Marekani bilioni 60 kwa mwaka katika 2021, na linatarajiwa kukua kwa zaidi ya asilimia saba kila mwaka hadi 2030, kulingana na data kutoka kwa Utafiti wa Polaris Market.

Lakini kwa nini afya ya utumbo ni muhimu na tunawezaje kuuimarisha?

Afya ya utumbo ni nini?

Si rahisi kutambua utumbo wenye afya kutokana na muundo wake ukilinganisha na viungo vingine, na hakuna chombo kimoja ambacho kinaweza kutumika kupima afya ya utumbo.

Utumbo wetu umejaa vijidudu. Kulingana na wataalamu vijidudu hivyo vikiwekwa pamoja, vinaweza kuwa na uzito zaidi ya kilo 1.8.

Kuna bakteria bilioni 100 katika kila gramu ya yaliyomo kwenye matumbo.

Utumbo wenye afya huelekea kuwa na jamii tofauti zaidi ya vijidudu, anasema Dk Katerina Johnson, ambaye anatafiti uhusiano kati ya utumbo na ubongo katika Chuo Kikuu cha Oxford.

Lakini, sayansi ya microbiome bado inaendelea kukua, anaongeza, akimaanisha kuwa hatujui kwa undani jinsi utumbo wenye afya unavyoonekana.

Kwa nini ni muhimu kuwa na utumbo wenye afya?

Mchoro wa urumbo

Chanzo cha picha,Getty Images

Utumbo unaweza kuathiri “karibu kila kiungo mwilini”, anasema Dk Johnson.

Ubongo na utumbo vina mfumo dhabiti wa mawasiliano unaojulikana kama mhimili wa utumbo na ubongo.

Viungo hivi vinategemeana na kila moja ni muhimu kwa nyingine - tafiti zimegundua kuwa ukuaji wa ubongo unaweza kuathika microbiome ya matumbo ikikosekana.

Utumbo wakati mwingine huitwa ubongo wa pili kwa sababu bakteria wanaweza kuathiri mienendo yetu kupitia Neurons milioni 100 kwenye utumbo.

Neurons ni seli zinazopatikana katika ubongo wetu na mfumo mkuu wa neva ambao huelekeza mwili wetu jinsi ya kuishi.

Utumbo wa nje unaweza hata kudhibiti hali yetu kwa kutoa vipitishio vya mawasiliano vinavyopatikana kwenye ubongo, kama vile serotonin.

kielelezo cha ubongo na utumbo unavyohusiana

Chanzo cha picha,Getty Images

Jukumu linalojulikana zaidi la utumbo ni kufyonza virutubisho kutoka kwa chakula.

"Hatuwezi kuwa tunapoteza maji na madini kwenye kinyesi," anaelezea Dk Venkatraman Krishna, daktari wa magonjwa ya tumbo nchini India.

Dk Megan Rossi, anayejulikana pia kama Daktari wa Afya wa Utumbo nchini Uingereza, anasema kukosekana kwa vijidudu vya utumbo sasa kumehusishwa na zaidi ya hali 70 tofauti za kiafya - kutoka magonjwa ya moyo, mishipa ya kupumua hadi magonjwa ya kinga ya mwili kama ugonjwa wa arheumatoid arthritis.

Takribani 70% ya seli zetu za kinga huishi kwenye sehemu ya utumbo, na "huwasiliana ya mara kwa mara" na mfumo wa kinga, anasema Dk Rossi.

Hii ndiyo sababu "watu walio na afya bora ya utumbo wanaonekana kuwa na mifumo ya kinga inayostahimili magonjwa zaidi", anaongeza.

Unawezaje kuimarisha afya ya utumbo?

Kufuatia utafiti uliofanywa na Mradi wa American Gut 2018, wataalamu walianza kuwashauri watu kula walau aina 30 ya lishe inayotokana na mimia kila wiki ili kukuza bakteria wanopatikana kwenye utumbo.

Hii sio tu ni pamoja na matunda na mboga, lakini pia vitu kama mbegu, viungo na karanga.

picha ya matunda na mboga

Chanzo cha picha,Getty Images

Dk Rossi anashauri watu kuongeza matunda katika lishe ili kuimarisha afya ya utumbo.

Lishe yenye nyuzinyuzi nyingi hutusaidia kujisikia kamili, husaidia usagaji chakula na kuzuia kuvimbiwa, kulingana na Huduma ya Kitaifa ya Afya ya Uingereza, ambayo inapendekeza watu wazima kula gramu 30 ya nyuzi kwa siku.

Kuchagua mikate ya unga au punje badala ya nyeupe, na kuchagua wali wa kahawia au pasta ya ngano, kunaweza kuongeza ulaji wako wa nyuzi.

 picha ya vyanzo vyema vya nyuzinyuzi kama vile mikate ya unga na pasta ya ngano

Chanzo cha picha,Getty Images

Chanzo kingine cha nyuzinyuzi ni pamoja na viazi ambavyoo havijamenywa (kama vile viazi vilivyookwa) na kunde kama maharagwe, dengu au mbaazi, ambazo zinaweza kuongezwa kwenye kitoweo, kari na saladi.

Vyakula vya prebiotic (aina fulani za nyuzi na wanga) vimepatikana ili kuhimiza ukuaji wa bakteria rafiki kwenye utumbo.

Baadhi ya vyakula hivyo ni ndizi, vitunguu, kabichi, nafaka, na zabibu.

Dk Hanisha Khemani, mtaalam wa magonjwa ya tumbo nchini Pakistan, anasema kuanzisha "mlo uliosawazishwa, na wenye virutubisho" katika miaka yetu ya 20 ni "muhimu kwa afya ya muda mrefu".

Ni vyakula gani mbaya kwa utumbo

Matumizi ya vyakula vilivyochakatwa sana, pombe na tumbaku si mazuri kwa utumbo wako, aeleza Dk Krishna.

Chakula kilichochakatwa sana kina viambato ambavyo ama hukandamiza bakteria 'nzuri' au kuongeza bakteria 'mbaya'.

photo off ultra processed corn puffs

Chanzo cha picha,Getty Images

Kwa kuzingatia mahali ulipo ulimwenguni, huenda ukalazimika kuacha kununua vyakula kutoka kwa wachuuzi wa mitaani wasiozingatia usafi hasa wa kuosha matunda na mboga ili kujikinga dhidi ya virusi au bakteria hatari, Dk Krishna anaongeza.

Anasisitiza uchafua matumbo yetu, na inaweza kuongeza asidi na vidonda vya tumbo.

Dkt Johnson anasema watu walio na mfadhaiko zaidi huwa na vijidudu vidogo vya aina mbalimbali.

 picha za vyakula vyenye afya kwa utumbo ikijumuisha matunda, mboga mboga na vyanzo vya nyuzinyuzi

Chanzo cha picha,Getty Images


Post a Comment

0 Comments