Moja ya taarifa iliyowapa butwaa mashabiki wa hip hop duniani hii ni baada ya rapa kanye west kutangaza rasmi kustaafu muziki.
Taarifa hii imethibitishwa na rapa @richthekid baada ya ku-share text za kanye akidai kuwa anastaafu muziki na hana hakika ni kipi kingine cha kufanya
“ninastaafu muziki, sina hakika ni kipi kingine nifanye” – kanye
“unastaafu!!…. kwanini, kivipi ?… watu wanakuhitaji, kwani muziki ambao tuliutengeneza mimi, wewe na ty dolla sign ulikuwa ni alama kubwa kwenye utamaduni (hiphop) hadi leo hii” – rich the kid akimjibu kanye
baadhi ya mashabiki twitter wameshangazwa na taarifa hiyo ya kanye kuacha muziki wakidai kuwa; kamwe sikuwahi kufikiria kama kanye atakuja kutumia neno “kustaafu” katika maisha”
“hivyo ndivyo inavyotokea pale ambapo watu hawakuheshimu tena, ila kama ni kweli basi
inabidi awe anatajwa kama wakali wa muda wote (g.o.a.t) 🐐” – shabiki
Baadhi ya mashabiki wamempuuza wakijua tu huenda ni kiki zake za kutaka kuwateka mashabiki kwenye soko la muziki kwa lengo la kuachia album ijayo au kazi yoyote mbeleni
kustaafu kwake kunaashiria mwisho wa enzi muhimu ya hip hop kwa msanii huyu, lakini pia mwanzo wa uwezekano mpya kwa mmoja wa watu wenye nguvu zaidi katika burudani duniani
Hii sio mara ya kwanza kwa kanye kutangaza hili kwani mwaka 2019 aliwahi kuwaambia mashabiki zake kuwa hatafanya tena muziki wa kidunia bali anajikita kwenye muziki wa injili tu.
wakati wa listening party ya albamu yake mpya ya “jesus is king” aliwaambia watu waliohudhuria kuwa, kwa sasa hatafanya tena muziki wa kidunia.
Kama shabiki wa muziki wa rapa Kanye West ni yapi maoni yako juu yauamuzi wake?
0 Comments