JSON Variables

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Alhamisi, 10 Julai 2025

WATANZANIA WATAKIWA KUTUMIA NISHATI SAFI


Charles Barnabas Kiongozi wa Ubia na Uhusiani wa Mradi wa masuala ya Nishati wa Services Modern Energy Cooking ambao unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uingereza (UKAD) kupitia ubalozi wa Uingereza Tanzania aki akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es salaam leo tar 10 July 2025.

Mwakilishi wa Kampuni inayojishughulisha na matumizi ya nishati safi majiko ya kutumia umeme SESCOM Shabani Selemani  akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es salaam leo tar 10 July 2025

...................

NA MUSSA KHALID

Watanzania wametakiwa kuepukana na matumizi ya kuni na mkaa badala yake watumie nishati safi ili kuendana na adhma ya serikali ya awamu ya sita ya mapambano ya mabadiliko ya tabia nchi.   

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Charles Barnabas Kiongozi wa Ubia na Uhusiani wa Mradi wa masuala ya Nishati wa Services Modern Energy Cooking ambao unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Uingereza (UKAD) kupitia ubalozi wa Uingereza Tanzania wakati wakifanya mradi wa Pikasmati katika eneo la Mwenge.

Amesema kuwa wanafanya kampeni ya mradi wa Pikasmati lengo lake ni kuongeza uelewa kwa wananchi kutumia matumizi ya nishati safi kwa kupika kwa umeme ili kuendana na dhamira ya serikali ya matumizi ya nishati safi.

“Tunawapa elimu wananchi watambue kwamba kupika kwa umeme sio gharama kubwa kwani kuna majiko ambayo ni fanisi kwa ajili ya matumizi hayo na elimu hii ndio imekuwa ikifanya watu waweze kutambua matumizi sahihi ya nishati safi ya kupikia’amesema Charles

Kwa upande wake Mwakilishi wa Kampuni inayojishughulisha na matumizi ya nishati safi majiko ya kutumia umeme SESCOM Shabani Selemani amesema matumizi yake yanasaidia kuonda  gharama na kupunguza uharibifu wa mazingira.

Nao baadhi ya wananchi Anamery George kutoka Kigamboni Twangoma na Oliver  John Mkazi wa Ubungo wameelezea umuhimu wa matumizi ya  nishati safi ya kupikia inasaidia katika utunzaji wa mazingira lakini pia inatunza muda sambamba na kuokoa gharama.

 Imeelezwa kuwa Kampeni hiyo ya Pikasmati ni ya Kitaifa ambayo inajumuisha maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Zanzibar ambapo itafanyika mpaka mwezi wa 12 mwaka huu ili watanzania wafahamu kuwa kupikia kwa umeme ni nafuu.

 

TFRA YAANZISHA MAABARA YA UPIMAJI WA UDONGO NA UBORA WA MBOLEA

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibi wa Mbolea Tanzania –(TFRA) Joel Laurent  akimsikiliza Afisa Udhibiti ubora Mwandamizi kutoka katika Mamlaka hiyo  Azizi Mtambo alipotembelea banda la Mamlaka hiyo katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya biashara 'Sabasaba' yanayoendelea jijini Dar es salaam leo tar 10/7/2025.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibi wa Mbolea Tanzania –(TFRA) Joel Laurent (kushoto) akimsikiliza Meneja wa Uhusiano, Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa TFRA, Bi. Matilda Kasanga (kulia) alipotembelea banda la Mamlaka hiyo katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya biashara 'Sabasaba' yanayoendelea jijini Dar es salaam leo tar 10/7/2025

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibi wa Mbolea Tanzania –(TFRA) Joel Laurent akimsikiliza Afisa kutoka TARI alipotembelea Banda la Taasisi hiyo katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya biashara 'Sabasaba' yanayoendelea jijini Dar es salaam leo tar 10/7/2025

.............................

NA MUSSA KHALID

Mamlaka ya Udhibi wa Mbolea Tanzania –TFRA imewasisitiza watanzania kutumia fursa ya uwepo wa maabara ya kisasa iliyoanzishwa na Mamlaka hiyo ili kujua afya ya udongo na ubora wa mbolea kuwa katika kiwango sahihi.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TFRA Joel Laurent wakati alipotembelea banda la Mamlaka hiyo katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya biashara 'Sabasaba' yanayoendelea jijini Dar es salaam ambapo amesema ni vyema wakaondoa wasiwasi kwani maabara hiyo inakwenda kuwasaidia katika shughuli zao za kilimo

Mkurugenzi huyo amesema kuwa lengo lao ni kuonyesha fursa zilizopo katika mnyororo wa thamani katika mbolea lakini pia kuwaelimisha watanzani namna ya kutumia matumizi sahihi ya mbolea.

Amesema mpaka kufika mwaka 2030 matumizi ya mbolea yatakuwa mara mbili ya kiwango cha sasa hivyo wameendelea kuyashawishi makampuni mbalimbali yaweze kuzalisha.

‘Mipango yetu ni kuendelea kuwa na mbolea sahihi kwa matumizi sahihi kwa wakulima wetu ambapo inatokana na wizara ya Kilimo kuendelea kupima afya ya udongo nchi nzima hivyo tunahitaji wenzetu wanaozalisha waweze kuagiza mbole ambazo zinaendana na afya ya udongo ili kuongeza tija’amesema Laurent

Aidha Laurent amesema kuwa Mamlaka hiyo imeanzisha mfumo wa kielekroniki ili wakulima waweze kujisajili jambo litakalosaidia wapate manufaa ya mbolea kwa bei himilivu.

Mkurugenzi huyo wa TFRA pia amesema kwa mwaka huu wameandaa mpango maalum wa kuongeza  uzalishaji wa mbolea kwa viwanda vya ndani kwa ajili ya wakulima ili ziweze kupatikana mapema,kwa urahisi na bei nafuu zaidi.

      

Jumatano, 9 Julai 2025

WATU ZAIDI YA LAKI 6 WATEMBELEA BANDA LA MALIASILI, SABASABA 2025

 

.................

Na Sixmund Begashe 

Witikio wa watu kwenye Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii kwenye Maonesho ya Biashara ya 49 ya Kimataifa yajulikanayo kama SABASABA umezidi kuwa mkubwa kutokana na mvuto wa huduma nzuri zinazotolewa na Idara na Taasisi zake, na kwa mujibu wa Bodi ya Utalii nchini hadi tarehe 8 Julai 2025, watu zaidi ya  laki 6 na sitini wameshatembelea banda hilo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania, Afisa Masoko Mwandamizi Bi. Flaviana Moshi amebainisha kuwa witikio huo unatokana na maandalizi mazuri yaliyofanywa na Wizara hiyo kupitia Bodi ya Utalii. 

Ameongeza kuwa licha ya huduma zingine wanazozipata kwenye Idara na taasisi za Wizara kama za utafiti, Malikale  pia kwenye banda hilo watu wanafanya Utalii wa Wanyamapori hai, wanapata bidhaa za Misitu na nyuki.

Naye Mzee Rashidi Jumanne, mkazi wa Bangala amesema licha ya kuwaona wanyama, amefurahishwa na utaratibu wa Wizara hiyo kuhakikisha watu wanapata huduma ya nyama ya Wanyamapori,  na vyakula mbalimbali.

"Nimefundishwa pale kwenye meza ya Chuo cha Utalii namna ya maandalizi ya meza ya chakula kwa wageni, nimekula nyama choma ya swala, nimeondoka na miche yangu ya miembe, naenda kupanda nyumbani". Alisema mzee Rashidi

Maonesho hayo ya SABASA yalianza tarehe 28 Juni 2025 na yanatarajiwa kufikia tamati tarehe 13 Julai 2025.







RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ASHIRIKI MKUTANO WA JARIDA LA UONGOZI LA AFRIKA

Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ameshiriki katika Mkutano Mkuu wa Afrika ulioandaliwa na Jarida la Uongozi la Afrika (African Leadership Magazine) na Taasisi ya Uongozi wa Afrika (African Leadership Organization) jijini London, Uingereza. 

Mkutano huo unazungumzia masuala mbalimbali ya Afrika, ikiwemo Uongozi, Uwekezaji na Ushindani wa Kimaendeleo kwa kauli mbiu ya: “Powering Leadership, Investment and Competitiveness”.

Awali, Mheshimiwa Rais Mstaafu ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Washauri ya African Leadership Organization (ALO), aliongoza vikao vya Bodi hiyo ambayo inaangazia masuala mbalimbali ya maendeleo ya Afrika kijamanii na kiuchumi. 

Bodi hiyo ina wajumbe kutoka nchi mbalimbali duniani, akiwemo Mhe. Dkt. Jewel Howard Taylor, Makamu wa Rais Mstaafu wa Liberia; Prof. Tahir Akhtar, Mkurugenzi wa Kampuni ya Adam Global Holdings UK/UAE; Dkt. Victor Oladukon, kutoka Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB); Dkt. Christian Lindfeld, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Africa Ventures Advisory - Germany; Jenerali William Kip Ward, Kamanda Mkuu Mstaafu wa Kamandi ya Jeshi la Marekani barani Afrika; Mhe. Nomvula Makonyane, Makamu Katibu Mkuu wa ANC - Afrika Kusini; na Dkt. Ken Giami, Mtendaji Mkuu wa African Leadership Organization (ALO). 

MAITI YA BINADAMU YATUMIKA KATIKA USAFIRISHAJI WA DAWA ZA KULEVYA

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini –DCEA akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo Julai 9,2025
......................

NA MUSSA KHALID

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini –DCEA inandelea kuwadhibiti baadhi ya wahalifu wa Dawa za kulevya ambao wameanza kutumia maiti za Binadamu kubeba dawa hizo maarufu kwa jina la begi ili kukosemsha uhalifu huo.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo Aretas Lyimo amebainisha hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wanahabari akitoa taarifa ya operesheni waliyoifanya kwa kipindi cha mwezi Mei hadi Julai mwaka huu.

Kamishna Jenerali Lyimo amesema wamebaini kumekuwa na matukio ya raia wa kigeni kuwatumia watanzania kusafirisha na kusambaza dawa za kulevya kwa kutumia njia hizo hivyo amewasisitiza wananchi kuwa makini na kuchukua tahadhari wanapotumwa au kupokea mizigo.

‘Mara niyingi huanzisha mahusiano ya kirafiki na kisha kuwahusisha katika biashara hii haramu kwa kutumia kampuni zao na vyombo vyao vya usafiri hususani bodaboda,bajaji,Tax na wasambazaji wa vifurushi’amesema Kamisha Lyimo

Aidha Kamishna Jenerali Lyimo amesema katika operesheni hizo pia wamekamata dawa za kulevya jumla ya Kilogram 37,197.142 na watuhumiwa 64 waliohusishwa na dawa hizo.

Amesema kuwa Dawa hizo zinajumuisha kilogram 11,031.42 za dawa mpya za kulevya aina ya Mitragyna Speciosa,bangi kilogram 24,873.56,mirungi kg 1,274.47,skanka kg 13.42,heroin kg 2.21 na methamphetamine gramu 1.42.

Ameendelea kueleza kuwa katia ukamataji huo umehusisha dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya ketamine kilogramu 1.92,Fluni-trazepam vidonge 1000,lita 6 za kemikali bashirifu aina ya hydrochloric acid na uteketezaji wa ekari 1,045.5 za mashamba ya bangi.

Kamishna Lyimo amesema katika mkoa wa Dar es salaam eneo la Sinza waliwakamata watu wawili wamiliki wa kiwanda bubu kinachotengeneza biskuti zinazochanganywa na bangi kisha kuzisambaza katika mikoa ya Dar es salaam,Mwanza,Lindi na Mtwara amba pia wakati huohuo mkoani Lindi alikamatwa mfanyabiashara wa madini akisambamba biskuti zilizochanganywa na bangi.

‘Vilevile kwa upande wa dawa za kulevya za mashambani zilikamatwa jumla ya Kilogram 26,191.45 za bangi,mirungi,skanka na kuteketeza akari 1,045.5 za mashamba ya bangi katika mikoa ya Ruvuma,Mbeya,Mara,Kagera,Dodoma,Tabora,Morogoro na Arusha. 

Hata hivyo Mamlaka hiyo imetoa tahadhari kwa mtu yeyote atakayeendelea kujihudisha na biashara,usambazaji na uzalishaji wa Dawa za Kulevya kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria pindi atakapobainika.

Jumanne, 8 Julai 2025

TANZANIA KOREA KUFANYA MRADI WA UPANUZI WA MFUMO WA GOTHOMIS

lNa Angela Msimbira, Seoul, Korea 

Serikali ya Korea Kusini kupitia shirika la KOICA imeandaa Mkutano wa Kimataifa kubadilishana uzoefu kwenye kuboresha mifumo ya usimamizi wa huduma za afya kwa kutumia teknolojia ya kisasa. 

Mkutano huu umehusisha watalaam kutoka Tanzania na Korea ikiwa ni sehemu ya ushirikiano wa Mradi wa Kupanua matumizi ya Mfumo wa GOTHOMIS unaotelekelezwa Mkoani Dodoma.

Akizungumza kwa niaba ya ujumbe wa Tanzania, Mkurugenzi Msaidizi - (Huduma za Lishe) Bw. Lutifrid Nnally, amesema ushiriki wa Tanzania unalenga kujifunza uzoefu wa Korea kwenye matumizi ya mifumo ya kidijitali katika huduma za afya.

Tanzania inatarajia kutumia uzoefu huo kufanya maboresho ya GOTHOMIS, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa kutumia teknolojia kama telemedicine, akili bandia (AI) na mifumo ya taarifa za kiafya.

Ushiriki huu ni hatua muhimu katika mageuzi ya sekta ya afya, hasa kwa maeneo ya vijijini, ili kuhakikisha huduma bora, za haraka na kwa gharama nafuu zinawafikia wananchi wote 

RAIS SAMIA APOKEA TUZO YA POWER OF 100 WOMEN AWARD KUTOKA ACCESS BANK GROUP

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Tuzo Maalum ya ‘Power of 100 Women Award mara baada ya kukabidhiwa Ikulu Jijini Dar es Salaam 08 Julai, 2025.

ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Access Tanzania Ndugu Protase Ishengoma pamoja na ujumbe aliombatana nao Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Julai, 2025.

Jumatatu, 7 Julai 2025

RAIS WA ZANZIBAR ATEMBELEA BANDA LA ETDCO KWENYE MAONESHO YA 49 YA SABASABA

wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO) wakiongozwa na Kaimu Meneja, CPA. Sadock Mugendi wakimkabidhi zawadi  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa, Dar es Salaam Sabasaba leo Juni 7, 2025 na kujionea jinsi  inavyotekeleza miradi mbalimbali ya umeme nchini (PICHA NA NOEL RUKANUGA)

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bw. Lazaro Twange (kulia) akisalimiana na Kaimu Meneja Kampuni ya ETDCO CPA. Sadock Mugendi wakati akitembelea banda la kampuni hiyo lililopo ndani ya Banda la TANESCO  katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa, Dar es Salaam Sabasaba.

Afisa Uhusiano wa Kampuni ya ETDCO Bi. Samia Chande akitoa elimu kwa wananchi kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme.Kaimu Meneja Kampuni ya ETDCO, CPA Sadock Mugendi, akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo leo, Julai 7, 2025, katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam.

.....

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo 7 Julai 2025, ametembelea banda la Kampuni ya ETDCO katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa, Dar es Salaam na kujionea namna Kampuni hiyo inavyotekeleza miradi mbalimbali ya umeme nchini.

Akiwa katika banda hilo, Mhe. Rais Dkt. Mwinyi amekabidhi zawadi ya sikukuu ya Sabasaba kwa wafanyakazi wa ETDCO wakiongozwa na Kaimu Meneja wa Kampuni hiyo, CPA. Sadock Mugendi.

Akizungumza na kuhusu na ushiriki wao katika maonesho hayo, CPA. Mugendi amesema kuwa lengo la ETDCO kushiriki meonesho ya sabasaba ni kuonesha utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya umeme nchini.

CPA. Mugendi ameeleza kuwa Kampuni hiyo imefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya usafirishaji umeme, ikiwemo mradi wa kusafirisha umeme wa kilovolti 132 kutoka Tabora hadi Katavi, ambao umewezesha wananchi wa maeneo hayo kupata umeme wa uhakika.

Aidha, amebainisha kuwa wameweza kukamilisha mradi mwingine wa kilovolti 132 kutoka Tabora Mjini hadi Urambo, wenye urefu wa kilomita 115, umeendelea kuimarisha upatikanaji wa umeme katika Mkoa huo.

"Tunawakaribisha wananchi wote kutembelea banda letu la ETDCO lililopo ndani ya banda la TANESCO. Lengo letu ni kuwaonesha wadau namna tunavyotekeleza miradi mbalimbali ya umeme kwa lengo la kuhakikisha watanzania wanafikiwa na huduma nchi zima," amesema CPA. Mugendi.

Ameongeza kuwa kampuni hiyo imefanikiwa kutekeleza miradi ya REA katika Mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Arusha, Katavi, Mbeya, Geita, pamoja na Kigoma.

CPA. Mugendi ameeleza kuwa utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa kusafirisha umeme kutoka Urambo – Nguruka – Kigoma, utakuwa wa kilovolti 132 wenye urefu wa kilomita 260.

Ameongeza kuwa mafanikio haya ni matokeo ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita, inayolenga kuhakisha watanzania wanafikiwa na huduma bora ya umeme nchini.

Mwisho.

Listen Mkisi Radio