JSON Variables

Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Jumatatu, 9 Juni 2025

CP. WAKULYAMBA AWAPA SOMO ASKARI WA JU.

...............

Na Sixmund Begashe, Katavi

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshughulikia masuala ya Uhifadhi, Kamishna wa Polisi (CP) Benedict Wakulyamba, ametoa semina elekezi kwa Maofisa na Askari Wanafunzi wa Kozi ya 11 ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), katika Kituo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Mlele, mkoani Katavi.

Katika semina hiyo, CP Wakulyamba amesisitiza masuala muhimu yanayohusu utendaji kazi wenye weledi, mahusiano bora kazini, madhara ya utendaji mbovu, pamoja na kazi za msingi za uhifadhi wa maliasili.

Aidha, amewahimiza Maofisa na Askari hao kujiepusha na vitendo vya rushwa na maadili mabovu kazini, huku akiwataka wajikite kujifunza na kuelewa vyema sheria husika, hasa zile zinazohusu uhifadhi wa maliasili.

“Ni lazima mjiepushe na utendaji mbovu. jiepusheni na rushwa, mjenge mahusiano mema na wananchi. Mkitaka kufanikisha majukumu yenu, mshirikiane kwa karibu na wananchi hao,” amesisitiza CP Wakulyamba.

Semina hiyo ni sehemu ya maandalizi kuelekea kufungwa kwa mafunzo rasmi ya Maofisa na Askari 229 wa Jeshi la Uhifadhi (JU) kutoka TANAPA kesho Juni 10, 2025 katika kituo hicho cha Mlele.

 

UKATILI DHIDI YA WATOTO NA VIJANA WAPUNGUA: WAZIRI DKT. GWAJIMA


....................
Na WMJJWM-Dar Es Salaam 

📌 Serikali yaahidi kutumia matokeo hayo kupanga mikakati na mipango na programu mbalimbali ya Serikali za kupambana na Ukatili.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema matokeo ya Utafiti wa Ukatili dhidi ya Watoto na Vijana wa mwaka 2024 yanaonesha Ukatili umepungua ukilinganisha na Utafiti kama huo uliofanywa Mwaka 2009.

Dkt. Gwajima ameyasema hayo wakati akitangaza matokeo ya utafiti huo Juni 9, 2025 Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Gwajima amesema, utafiti huo unaonesha kupungua kwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto wa kike ambapo, ukatili wa kingono umepungua kutoka asilimia 33 hadi asilimia 11,  Ukatili wa kimwili umepungua kutoka asilimia 76 hadi asilimia 24 na Ukatili wa kihisia umepungua kutoka asilimia 25 hadi asilimia 22.

Aidha, kwa watoto wa kiume, Ukatili wa kingono umepungua kutoka asilimia 21 hadi asilimia 5, Ukatili wa kimwili umepungua kutoka asilimia 74 hadi asilimia 21 na Ukatili wa kihisia umepungua kutoka asilimia 31 hadi asilimia 16.

"Naomba mfahamu kuwa, huu ni utafiti wa Pili wa kitaifa ambao umefanyika baada ya miaka 15 tangu utafiti ule wa kwanza wa mwaka 2009. Matokeo ya utafiti yanaonesha ukatili umeshuka kwa kiwango kikubwa ukilinganisha utafiti wa 2009 na huu wa 2024" amesema Dkt. Gwajima

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum itafanya tathmini, mapitio na maboresho ya Sera na Sheria zilizopo, sambamba na uimarishaji wa programu za kisekta za kuzuia na kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya makundi yote kwa kufanya uchambuzi wa afua zilizoainishwa katika MTAKUWWA wa Pili na kulinganisha na matokeo ya utafiti huu wa pili na hili litasaidia katika kuongeza bajeti na rasilimali watu ili kuzuia ukatili dhidi ya makundi yote na kuboresha huduma kwa manusura wa vitendo vya ukatili.

"Ninaomba kusisitiza kuwa, matokeo haya ya utafiti huu yatawezesha Serikali na Wadau kuboresha na kuandaa Mipango, Programu na Mikakati mbalimbali ya kutokomeza ukatili nchini itakayoimarisha Ulinzi na Usalama wa Watoto na Vijana kwa maslahi mapana ya kizazi cha sasa na cha baadae." amesisitiza Dkt. Gwajima 

Dkt. Gwajima amesema, suala la ukatili dhidi ya watoto na vijana ni la ukiukaji wa haki za binadamu na pia linaleta changamoto kubwa za afya katika jamii na kubadilisha maisha ya watu wanaopitia ukatili. 

Ameongeza kwamba, ukatili huleta athari za muda mrefu za kiafya ikiwa ni pamoja na matatizo ya afya akili, mawazo ya kujiua, tabia hatarishi za ngono, uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa ya zinaa ikiwemo VVU, matumizi ya dawa za kulevya. Pia ukatili hupunguza fursa mbalimbali za kimaendeleo na kuongeza umaskini katika jamii.

Naye Mtakwimu Mkuu wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Amina Msengwa amesema, utafiti huo ni wa Kitaifa ambapo umefanywa katika mikoa 31 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia sampuli wakilishi ya Kitaifa hivyo, Takwimu hizo ni bora na zinafaa katika kuweka mipango mikakati na Programu na kufanya tathmini ya kuwalinda Watoto na Vijana dhidi ya Ukatili.



MAKAMU WA RAIS AKISHIRIKI UFUNGUZI WA MKUTANO WA TATU WA BAHARI


....................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishiriki ufunguzi wa Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari (UNOC3), unaofanyika Jijini Nice nchini Ufaransa leo tarehe 09 Juni 2025. Kulia ni Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Shaaban Ali Othman.

MRADI WA KUZALISHA UMEME WA JUA KISHAPU WAFIKIA ASILIMIA 63.3 - MD TWANGE

.................

📌Asema awamu ya kwanza utazalisha Megawati 50 na kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Bw. Lazaro Twange amesema Mradi wa uzalishaji umeme unaotokana na jua wa Kishapu Mkoani Shinyanga umefikia asilimia 63.3 kukamilika ambapo amesema awamu ya kwanza ya Mradi huo utazalisha Megawati 50 ambazo zitaingizwa kwenye gridi ya Taifa ifikapo mwishoni mwa mwezi wa kumi mwaka huu.

MD Twange ameyasema hayo leo Juni 8 mwaka 2025 alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo ambao unagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 118 kwa awamu ya kwanza huku awamu ya pili ikitarajia kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 204.

‘’Kwanza tunamshukuru Mhe. Rais kwa kutupatia fedha kwa awamu zote, kama mnavyoona kazi inaendelea na Mradi unatarajia kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa mwishoni mwa mwezi wa kumi kwa ajili ya kuwasambazia umeme wananchi, lakini pia tuko katika hatua za mwisho za manunuzi kwa ajili ya kumpata mkandarasi atakayetekeleza Mradi kwa awamu ya pili ambayo itazalisha megati 100’’ alisisitiza Mkurugenzi Mtendaji Twange.

Aidha, amewahakikishia wananchi kuwa TANESCO inafanya jitihada za makusudi za kuhakikisha Mradi unakamilika kwa wakati ili kuendana na ongezeko la mahitaji ya watu na shughuli za uwekezaji ambazo zinategemea nishati ya umeme kujiendesha.

Naye Meneja wa Mradi huo Mhandisi Emmanuel Andarson amesema awali Mradi huo ulipaswa kukamilika mwezi February mwaka huu lakini Mkandarasi aliongezewa muda baada kukabiliwa na baadhi ya changamoto ambapo ameahidi kukamilisha Mradi huo kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba .

Mradi wa uzalishaji wa umeme unaotokana na nguvu ya jua wa Kishapu uliopo katika Kijiji cha Ngunga Mkoani Shinyanga ulianza utekelezaji wake Desemba 8 mwaka 2023 na unatarajia kukamilika rasmi Oktoba 29 2025 ambapo unagharimu jumla ya shilingi bililioni 323 kwa awamu zote mbili ukitarajia kuzalisha megawati 150 za umeme.


Ijumaa, 6 Juni 2025

MWANDUMBYA ATETA NA UJUMBE WA KAMPUNI YA ALSTOM

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ALSTOM, nchini Tanzania, inayojihusisha na uwekezaji katika ujenzi na uendeshaji wa miundombinu ya reli duniani,  Bi.  Kefilwe Mothupi, baada ya kumalizika kwa kikao kilichofanyika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), Bw. David Kafulila, baada ya kumalizika kwa kikao na Ujumbe kutoka Kampuni ya ALSTOM, kilichofanyika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini, Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Elijah Mwandumbya, akiongoza kikao na ujumbe wa Kampuni ya ALSTOM, ambapo pamoja na mambo mengine walijadiliana kuhusu uendelezaji wa miundombinu jijini Dar es Salaam, kikao hicho kilifanyika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini, Dodoma.

Mkurugenzi wa Miradi na Fedha, Ofisi ya ALSTOM, Bi. Julie Morel, akifanya wasilisho kuhusu utekelezaji wa mradi wa miundombinu jijini Dar es Salaam wakati wa kikao na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, kilichofanyika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini, Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)

................

Na. Josephine Majura, WF, Dodoma

 

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Kampuni ya ALSTOM, yenye Makao yake Makuu nchini Ufaransa, iliyoonesha nia ya kuwekeza katika ujenzi na uendeshaji wa miundombinu ya reli ili kupunguza msongamano wa magari na kuboresha usafiri  katika jiji la Dar es Salaam.

Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini, Dodoma na kuhudhuriwa na Kaimu Kamishna wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) Wizara ya Fedha, Bw. Bashiru Taratibu, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), Bw. David Kafulila, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sheria, Wizara ya Fedha, Bi. Zawadi Maginga pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Kampuni ya ALSTOM.


Alhamisi, 5 Juni 2025

MAKAMU WA RAIS AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI JUNI 05,2025

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Viongozi mbalimbali wakati alipowasili katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani tarehe 05 Juni 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Bi. Joyce Mnunguli kuhusu Mfumo Jumuishi wa Taifa wa Usimamizi wa Mazingira (E-Mazingira) wakati akikagua mabanda ya maonesho katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa maelekezo mbalimbali kwa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira wakati akikagua mabanda ya maonesho katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati Mhandisi Innocent Luoga kuhusu matumizi ya magari yanayotumia umeme ili kulinda mazingira wakati akikagua mabanda ya maonesho katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akishuhudia gari la usafi linalotumia umeme ili kulinda mazingira linalomilikiwa na Kampuni ya Suma JKT wakati akikagua mabanda katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma tarehe 05 Juni 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na viongozi mbalimbali wakiwa katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete wakishiriki Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani tarehe

05 Juni 2025.

......................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa kwa wadau wote wa mazingira kuendeleza mambo yote yaliyofanyika katika maadhimisho ya mazingira ikiwa ni pamoja na upandaji miti na uanzishwaji wa bustani za kijani.

Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani iliyofanyika Kitaifa katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Mkoani Dodoma. Amewahimiza wadau hao kuhamasisha matumizi ya teknolojia za urejelezaji wa taka ozo na za plastiki, kupunguza ukataji miti holela kwa ajili ya kuni na mkaa na kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Aidha, Makamu wa Rais amesema Serikali imeweka nia ya kupunguza athari za uharibifu wa mazingira kwa kupunguza matumizi ya nishati ya kuni na mkaa kwa shughuli za kupikia. Amesema katika kutekeleza nia hiyo, Serikali ilitoa katazo la matumizi ya kuni na mkaa kwa taasisi zinazoandaa chakula na kulisha watu zaidi ya watu mia moja kwa siku na kuzitaka zihamie katika matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo kufikia Machi 2025 jumla ya taasisi 762 zimeanza kutumia nishati safi ya kupikia kati ya hizo taasisi za umma ni 495 na taasisi binafsi ni 267.

Halikadhalika Makamu wa Rais amesema jukumu la kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa hifadhi ya mazingira linahitaji ushirikiano wa wadau wote katika ngazi zote. ametoa wito kwa vyombo vya habari, taasisi zote za Serikali, binafsi na asasi za kiraia kushirikiana katika kutoa elimu kwa jamii ili kupunguza uharibifu wa mazingira hapa nchini kwa kiasi kikubwa.

Makamu wa Rais amesema taarifa mbalimbali za hali ya mazingira nchini zimedhihirisha kuwepo kwa uharibifu wa ardhi katika maeneo mbalimbali nchini, ambapo inakadiriwa kuwa takriban asilimia 61 ya ardhi nchini iko katika hatari ya kuharibika. Amesema uharibifu huo unachangiwa kwa kiasi kikubwa na shughuli za kibinadamu zisizo endelevu, idadi kubwa ya mifugo isiyolingana na uwezo wa malisho, ukataji wa misitu kwa ajili ya kuni na mkaa, uanzishaji wa mashamba mapya unaotokana na kilimo cha kuhamahama, uchimbaji holela wa madini pamoja na upanuzi wa makazi usiozingatia mipango miji.

Makamu wa Rais amesema katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira, Serikali imechukua hatua mbalimbali za kisera na kimkakati ikiwa ni pamoja na kupitishwa kwa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021, Mpango Kabambe wa Taifa wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (2022-2032), kuongeza kasi ya upimaji wa ardhi na umilikishaji wa ardhi kimila.

Amesema hatua nyingine ni pamoja na uhamasishaji wa matumizi endelevu ya ardhi hususan kilimo mseto, kilimo cha matuta, kilimo hifadhi na mbinu endelevu za kiasili za hifadhi ya malisho. na utekelezaji wa hatua hizi ikiwa ni pamoja na kuendelea kuhamasisha utunzaji wa mazingira kwa ujumla.

Vilevile, Makamu wa Rais amewahimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwan kwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, kushiriki kampeni ili kusikiliza sera za wagombea na kujitokeza kupiga kura siku ya uchaguzi. Aidha amewasihi wananchi hususani vijana kudumisha hali ya utulivu na usalama hususan katika hatua ya uteuzi wa wagombea, kampeni za uchaguzi, upigaji kura na hata baada ya matokeo kutangazwa.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Khamis Hamza Khamis amesema kauli mbiu ya mwaka 2025 inahamasisha jamii kupunguza matumizi ya bidhaa za plastiki kwa kuwa na uzalishaji na ulaji endelevu kwa lengo la kuhifadhi mito, maziwa na bahari ili kuhifadhi mifumo ya ikolojia.

Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Kitaifa yamebeba kauli mbiu isemayo “Mazingira Yetu na Tanzania Ijayo, Tuwajibike Sasa: Dhibiti Matumizi ya Plastiki”.

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais

05 Juni 2025

Dodoma.

SERIKALI ITAENDELEA KUISIMAMIA SEKTA YA AFYA-MAJALIWA

.....................

▪️Ampongeza Rais Dkt. Samia kwa kuendelea kutoa vibali vya ajira sekta ya afya
 
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu itaendela kuisimamia na kuipa hadhi sekta ya afya ikiwemo kutoa vibali vya ajira pamoja na kujenga miundombinu ya kutolea huduma hizo katika ngazi zote.

Amesema mpango wa Serikali kwa sasa ni kuhakikisha huduma za afya zinatolewa kwa uhakika na kwa usahihi, ndio maana iliamua kuwa na mkakati wa kuwapeleka Watanzania kusoma katika vyuo mbalimbali ili waje kutoa huduma kwa wananchi.

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Alhamisi, Juni 5, 2025) wakati akijibu swali  Mbunge wa Viti Maalumu, Jackline Andrew aliyetaka kujua mpango wa Serikali katika kuhakikisha wilaya zote zinapata madaktari bingwa hadi ngazi za vituo vya afya kwa ajili ya kuhudumia mama na mtoto.

Amesema ajira hizo ambazo Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaruhusu kwa kutoa vibali kuweza kuwaajiri madaktari wakiwemo mabingwa wa magonjwa ya mama na mtoto, upasuaji ambao kwa sasa wanapelekwa hadi ngazi ya wilaya.“Tumewaagiza waganga wakuu wa mikoa kuhakikisha waangalia ikama ya madaktari bingwa na kuwapeleka kwenye maeneo yenye upungufu.”

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia kitengo cha maafa imeweka utaratibu wa kupata taarifa za maafa yoyote kuanzia ngazi za vijiji kupitia kamati za maafa zilizoundwa kuanzia ngazi ya kijiji hadi Taifa.

Amesema malengo la kamati hizo ni kubaini tatizo linapojitokeza na kuharakisha kutoa taarifa katika ngazi ya juu ili kusaidia utoaji wa taarifa na kueleza ukubwa wa tatizo na kuchukua hatua. 

Waziri Mkuu ameyasema hayo alipokuwa ajibu swali ya mbunge wa Momba, Condester Sichwale aliyetaka kufahamu kauli ya Serikali katika kukabiliana na maafa. “Kazi kubwa tunayoifanya sasa ni kuziimarisha kamati hizi kwa kuzipa elimu na mifumo inayoweza kutoa taarifa kwa haraka kwenda kamati za juu.”

Waziri Mkuu amesema maafa yanapotokea katika ngazi ya kijiji na wilaya, Mkuu wa Wilaya ndiye Mwenyekiti wa kamati ya maafa anachukua hatua na anapoona aina hiyo ya maafa imemzidi anatoa taarifa mkoani na baadae Taifa.

Waziri Mkuu amesema katika kuhakikisha taarifa zinafika kwa haraka Serikali imeamua kuanzisha maeneo ya kimkakati kwenye ngazi za kanda ambapo vifaa mbalimbali vya kukabiliana na maafa vimepelekwa ili iwe rahisi kuwasiliana na mkoa na kufika kwenye maeneo kwa wakati.

Jumatano, 4 Juni 2025

KIWANDA CHA KUSAFISHA NA KUONGEZA THAMANI MADINI ADIMU KUJENGWA KIJIJINI NGWALA,SONGWE

 

KIWANDA CHA KUSAFISHA NA KUONGEZA THAMANI MADINI ADIMU KUJENGWA KIJIJINI NGWALA,SONGWE


▪️Uendelezaji wa Mradi kuanza rasmi    Disemba 2025


▪️Ni mradi wa Madini Adimu utakaogharimu Bilioni 771


▪️Waziri Mavunde azindua zoezi la ulipwaji fidia wananchi 192


▪️Wananchi wamshukuru Rais Samia kwa mazingira ya uwekezaji


▪️Serikali kuvuna mapato ya zaidi ya Trilioni 12 


Ngwala,Songwe


Kampuni ya Mamba Minerals Ltd inayowekeza kwenye mradi wa Madini adimu imeweka wazi mpango wake wa kujenga kiwanda cha kusafisha na kuongeza thamani madini adimu kijijini,Ngwala Mkoani Songwe badala ya kusafirisha madini hayo yakiwa ghafi.


Hayo yamesemwa leo Kijijini Ngwala,Songwe wakati wa uzinduzi wa zoezi la ulipwaji fidia wananchi waguswa wa mradi takribani 192 zoezi ambalo limezunduliwa na Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde.

Akitoa maelezo ya awali,Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mamba Minerals Ltd Ndg. Ismail Diwani amesema zoezi hilo la fidia litagharimu kiasi cha Tsh 5.3 Bilioni kwa kuhusisha wananchi waguswa wa mradi 192 ambapo mpaka sasa wananchi 116 wamepokea malipo yao tayari.


“Hatua hizi ni za awali kuelekea kwenye utekelezaji wa mradi ambapo shughuli rasmi za ujenzi wa mradi zitaanza Disemba 2025 sambamba na ujenzi wa kiwanda cha kusafisha madini adimu na ujenzi wa mtambo wa kufua umeme utakaozalisha megawati 12”Alisema Ismail

Waziri Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Mamba Minerals Ltd kwa ujenzi wa kiwanda cha kusafisha madini hayo hapa nchin ikiwa ni uongezaji wa thamani wa madini hayo kabla ya kusafirishwa ikiwa ni sehemu ya kuitikia wito uliotolewa na Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan juu ya uongezaji thamani madini nchini.


“Mradi huu pamoja na Ajira,mrabaha,ushuru wa Halmashauri pia utaipa serikali mapato ya moja kwa moja ya zaidi ya Tsh 12 Trilioni wakati wote wa uhai wa mgodi.


Tutahakikisha wananchi wa Ngwala wananufaika na mradi huu mkubwa kupitia maudhui ya ndani(𝙡𝙤𝙘𝙖𝙡 𝙘𝙤𝙣𝙩𝙚𝙣𝙩) na hivyo mradi huu kuwa kichocheo cha maendeleo ya kiuchumi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Mradi huu una wastani wa mashapo ya  Tani 18.5 milioni  za madini adimu ni kati ya miradi mikubwa  duniani ya madini adimu na hivyo itaifanya Tanzania kuwa mzalishaji wa malighafi kwa ajili ya vifaa vya matibabu,kieletroniki na ufuaji wa umeme wa upepo”Alisema Mavunde


Naye Mkuu wa Wilaya wa Songwe Mh. Solomon Itunda amesema mradi huu utachochea ukuaji wa sekta ya madini Mkoani Songwe kwa kiwango kikubwa na hivyo kuufanya mkoa huu kuwa kati ya wachangiaji wakubwa katika kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya madini.

KAMPUNI YA KIZALENDO (MOFAT) YAULA MABASI YA ENDAYO HARAKA (BRT)


 Na Mwandishi wetu 


KAMPUNI ya Kizalendo ya Mofat imepewa mkataba wa miaka 12 na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Dart) kwa ajili ya kuendesha Awamu ya Pili ya mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT), unaotoka Gerezani hadi Mbagala. 


Kampuni hiyo ya Kizalendo ya Mofat inatarajiwa kuanza kutumia mabasi 255 yanayotumia gesi ifikapo Agosti 2025.

Akizungumza hayo hivi karibuni Mkurugenzi Mtendaji wa Dart, Dkt. Athuman Kihamia, alithibitisha kuhusu mkataba huo jana katika mahojiano ya simu akiwa nje ya nchi.


Alisema maendeleo yanakuja wakati serikali ikihamia rasmi katika kuhamisha uendeshaji wa awamu ya kwanza na ya pili ya mfumo wa BRT kwa sekta binafsi, ikiwa ni juhudi za kuongeza ufanisi na kushughulikia changamoto za muda mrefu za usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.

''Hii ni kampuni ya kizalendo na tayari imepata mitaji na dhamana zinazohitajika kuendesha huduma hii.


"Hivyo hii ni hatua kubwa katika juhudi zetu za kutoa huduma za usafiri wa uhakika na bora kwa wakazi wa jiji. Kampuni hiyo imejitolea kuleta mabasi ndani ya muda tuliokubaliana,"alisema Dkt. Kihamia.

Mwelekeo wa kuwashirikisha zaidi waendeshaji wa ndani ulisisitizwa pia Jumatatu na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, aliyewaambia wahariri jijini Dar es Salaam kuwa Dart sasa inalenga kuvutia wawekezaji zaidi—hasa kwa kuwa ujenzi wa Awamu ya Kwanza na ya Pili umekamilika, huku Awamu ya Tatu ikitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.


Kwa mujibu wa mfumo mpya, mfumo wa BRT utaendeshwa na kampuni kati ya nne hadi sita, badala ya mfumo wa sasa wa mtoa huduma mmoja unaoongozwa na UDA Rapid Transit (Udart).

Listen Mkisi Radio